BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
HATIMAYE Arsenal imepangua wingu zito lililokuwa limetanda mbele yao kwenye hatua ya makundi ya Champions League na kuichabanga Olympiacos 3-0 kwenye mchezo wa kundi F.
Ushindi huo umetosha kabisa kuivusha Arsenal kwenda hatua ya 16 bora ikiwa ni mwaka wa 16 mfululizo kutinga hatua hiyo.Shujaa wa Arsenal alikuwa ni mshambuliaji Olivier Giroud aliyefunga mabao yote matatu katika dakika ya 29 na 49 huku bao lake la tatu akifunga dakika ya 67 kupitia mkwaju wa penalti.

Arsenal ambao walikubali kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa Olympiacos walipocheza kwenye dimba lao la Emirates, Jumatano hii wakiwa ugenini kwenye uwanja wa Georgios Karaiskakis jijini Athens, Ugiriki, wakacharuka na kufanya kile kilichohitajika.

Ili kusonga mbele kwa tofauti ya mabao, Arsenal ilitakiwa ishinde kwa zaidi ya bao moja ili kuipiku Olympiakos.

Katika mchezo mwingine wa kundi F, Bayern Munich imeendeleza ubabe kwa kuichapa Dinamo Zagreb 2-0 mabao yote yakifungwa na Robert Lewandowski katika dakika ya 61 na 64.Olympiacos: Roberto 4, Elabdellaoui 5, Da Costa 5, Siovas 5, Masuaku 5, Kasami 5 (Dominguez 71, 5), Milivojevic 5, Seba 5 (Hernani 77, 5), Fortounis 6.5, Pardo 5 (Finnbogason 86), Ideye 5.

Arsenal: Cech 7, Bellerin 6.5, Mertesacker 7.5, Koscielny 7.5, Monreal 7, Ramsey 7.5, Flamini 7, Walcott 7 (Gibbs 72, 6), Ozil 9, Campbell 8.5 (Oxlade-Chamberlain 90), Giroud 9.5 (Chambers 90).


Post a Comment

 
Top