BOIPLUS SPORTS BLOG

LOUIS van Gaal sasa ni wazi amekalia kuti kavu baada ya kuendelea kupata matokeo mabovu baada ya leo vijana wa Manchester United kukubali kipigo cha mabao  2-1 nyumbani Old Trafford kutoka kwa  Norwich City –na ulikuwa mchezo wa nne katika ligi bila ushindi.


Man United ambao walianza vizuri mchezo huo, waliruhusu goli  kabla ya timu hizo kwenda mapumziko ambalo lilifungwa na  Cameron Jerome.

Vijana wa Alex Neil waliwashtua tena wenyeji kwa goli toka kwa  Alex Tettey  baada ya Man United kushindwa kimiliki mpira eneo la kati.


Anthony Martial, ambaye ndo kwanza ametoka kupokea tuzo ya  Golden Boy  kwa 2015, aliwafungia United goli dakika ya 67 baada ya kufumua shuti kufuatia piga ni kupige langoni mwa Norwich.

Hadi dakika 90 zinamalizika Man United 1-2 Norwich City na hivyo kuondoka na pointi 3, na kuwafanya United kuwa hawajapata ushindi wowote katika mechi 6.


Post a Comment

 
Top