BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga ya jijini Dar Es Salaam, leo imejinyakulia pointi tatu muhimu baada ya kuinyuka African Sports bao 1-0, mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Yanga waliotoka kuambulia sare ya bila mabao ilipopambana na Mgambo JKT, iliingia uwanjani ikiwa na kiu ya kupata ushindi kwa kulishambulia lango la Mgambo lakini umakini wa walinzi ulikuwa kikwazo.


Alikuwa ni kiungo Thaban Kamusoko ndiye aliyewanyanyua vitini mashabiki wa Yanga waliokuwa wameshakata tamaa,  baada ya kuifungia timu yake bao maridadi katika dakika za nyongeza za mchezo huo.

Kwa ushindi huo Yanga imechupa hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiipiku Azam Fc ambayo ina mchezo mmoja mkononi.

 Vikosi katika mchezo wa leo vilikuwa kama ifuatavyo;

YANGA
 Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Malimi Busungu, Donald Ngoma na Deus Kaseke/ Godfrey Mwashiuya.

AFRICAN SPORTS
Ramadhani Mwaluko, Mwaita Ngereza, Khalfan Twenye, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Mussa Chambega/Ally Ramadhani ‘Kagawa’,
Mussa Kizenga/James Mendi, Pera Ramadhani, Hassan Materema, Mohammed Mtindi/Hussein Issa na Mohamed Issa.

Post a Comment

 
Top