BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
JANA ilifanyika hafla ya utoaji tuzo za ligi kuu nchini Hispania 'La Liga' kwa msimu ulioisha wa 2014/2015.

Katika orodha iliyotangazwa, kocha wa FC Barcelona Luis Enrique aliibuka  mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwaka huku kiungo wa zamani wa timu hiyo, Xavi Hernandes akitajwa kuwa kiungo bora.

Golikipa Claudio Bravo wa FC Barcelona alitangazwa kuwa golikipa bora wa msimu wakati beki bora alikuwa ni Sergio Ramos wa Real Madrid ambaye aliibeba Real Madrid kwa kiwango kikubwa msimu uliopita.

Kinda wa kibrazil ambaye ametajwa pia katika wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia, Neymar alitwaa tuzo ya mchezaji bora kutoka bara la America

Kiungo James Rodriguez wa Real Madrid alitangazwa kuwa kiungo bora wa msimu na mchezaji bora wa Dunia, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2014/2015 huku pia  akishinda tuzo ya  mshambuliaji bora wa msimu huo.

Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye hakuhudhuria hafla hiyo aliambulia tuzo maalumu ya mashabiki, tuzo ambayo ilipokelewa na Ramos kwa niaba yake.

Post a Comment

 
Top