BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
USIKU wa jana Barcelona iliendeleza vipigo kwa kila timu inayokuja mbele yake huku jana ikiua 6-1  dhidi ya Villanovense mchezo uliopigwa katika dimba la Nou Camp.


Kwa sasa  Barcelona unaweza kuita ndio timu inayoongoza kwa safu bora ya ushambuliaji kutokana na kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli kwenye mechi zake za hivi karibuni.  Matokeo ya mechi zao nne zilizopita zinaonesha kuwa walimfunga Real Madrid 4-0 La Liga, wakamfunga AS Roma 6-1 UEFA, wakamfunga Real Sociedad 4-0, kabla ya jana  kuifunga Villanovense magoli 6-1 katika mchezo wa Copa del Rey.


Kwa takwimu hizo FC Barcelona wanakuwa wamefunga jumla ya mabao 20 katika mechi nne, ambapo ni sawa na wastani wa mabao 5 kwa kila mechi.


Katika mchezo wa jana, mabao ya FC Barcelona yamefungwa na Daniel Alves dakika ya 4, Sandro Ramirez dakika ya 21, 31, 69 na  Munir El Haddadi dakika ya 51 na 7 wakati goli pekee la Villanovense lilifungwa na Juanfran dakika ya 29.

Matokeo  ya michezo mingine ni Kama ifuatavyo

Spain - Copa del Rey

FT Barakaldo 1 - 3 Valencia
FT UD Logroñés 0 - 3 Sevilla
FT Almería 1 - 3 Celta de Vigo
FT Llagostera 1 - 2 Deportivo La Coruña
FT Real Betis 2 - 0 Sporting Gijón
FT Rayo Vallecano 2 - 0 Getafe
FT Cádiz 1 - 3 Real Madrid

Post a Comment

 
Top