BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA Moses Basena anatarajia kutua nchini kesho kwa ajili ya kujiunga na Simba kama msaidizi wa Dylan Kerr na mara baada ya kutua atasaini mkataba na klabu hiyo tayari kwa kuanza kazi.

Basena ambaye amewahi kuifundisha timu hiyo kama kocha mkuu na baadaye kuwa Mkurugenzi wa benchi la ufundi atakuwepo katika mechi yao na Azam itakayochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.


Kiongozi mmoja wa Simba ameiambia BOIPLUS kuwa mazungumzo ya awali na Basena yalifanyika lakini walikuwa wakimsubiri kumalizana naye kwa upande wa mkataba akitoka kwenye michuano ya Kombe la Chalenji ambapo timu yake ya Uganda 'The Cranes' ilitwaa ubingwa huo.

"Basena ataingia kesho maana tunahitaji awepo kwenye mechi yetu na Azam, atakuja na beki wetu Juuko Murshid ambapo wote walikuwa kwenye majukumu ya timu yao ya Taifa. Ila kila kitu kwa upande wa Basena kinakwenda vizuri," alisema kiongozi huyo.

Basena anakuja kuchukuwa mikoba ya Seleman Matola aliyeachia ngazi na sasa ni kocha mkuu wa timu ya Geita Gold Mine inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).


Post a Comment

 
Top