BOIPLUS SPORTS BLOG

RAIS wa FIFA, Sepp Blatter na Bosi wa UEFA Michel Platin wamefungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya kufanya malipo ya paundi 1.3 milioni kinyume na utaratibu.Wote wawili walikataa makosa hayo na hilo halikuzuia kutolewa kwa adhabu hiyo iliyoambatana na faini ambapo Blatter atatakiwa kulipa paundi 33,700 na Platini akilazimika kulipa paundi 54,000.

Platin ndiye aliyekuwa akitajwa kumrithi Blatter kwenye nafasi ya Rais wa FIFA kwenye uchaguzi ilutakaofayika mwezi februari mwakani, lakini kutokana na zuio hili hawezi tena kugombea.

Hadi sasa kuna wagombea watano kwenye kinyang'anyiro cha uraisi akiwemo Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa wa Bahrain, Tokyo Sexwale wa Afrika ya Kusini, Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan, katibu mkuu wa UEFA Gianni Infantino na Jarome Champagne wa Ufaransa.

Post a Comment

 
Top