BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KUMEKUCHA Msimbazi, baada ya mshambuliaji Raphael Modo Kiongera kugoma kutua nchini hadi hapo atakapomaliziwa pesa yake ya usajili pamoja na mishahara ya miezi miwili, hatimae Uongozi wa Wekundu wa Msimbazi umekamilisha kila kitu na Straika huyo amejiunga na wenzake Zanzibar.

Kiongera ambaye ametua Zanzibar majira ya saa mbili usiku huu, al├Čiambia BOIPLUS mwanzoni mwa wiki hii kuwa yupo tayari kuja kuitumikia timu yake lakini ni kwa sharti la kulipwa madai yake yote kwanza.


Imefahamika kwamba uongozi wa Simba ulijipinda jana na kumuingizia kwenye akaunti yake dola 10,000 ya deni la ada ya usajili pamoja na mishahara ya mwezi Juni na Novemba aliyokuwa akidai.

Kuwasili kwa Kiongera kunahitimisha tetesi zote za usajili wa mapro kutoka nje ya nchi kwavile tayari Simba inakuwa imetimiza idadi ya wacheza saba wa kigeni walioruhusiwa na TFF.

Wachezaji wa kigeni wa Simba ni Hamis Kiiza, Emery Nimubona, Vincent Angban, Juuko Murshid, Justice Majabvi,  Majwega na Kiongera aliyetua leo.

Post a Comment

 
Top