BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
HATIMAYE lile fumbo la muda mrefu kama wachezaji wapya wa Simba waliosajiliwa katika dirisha dogo watacheza mechi na Azam au la, limepata majibu. 



BOIPLUS imepenyezewa taarifa kutoka katika kikao cha kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji kilichomalizika dakika chache zilizopita kuwa kimeamuru timu zote za ligi zisiwatumie wachezaji wake wapya hadi baada ya Disemba 23 kamati hiyo itakapokaa na kupitia mapingamizi.

Kwa mantiki hiyo leo wekundu wa Msimbazi  Simba itashindwa kuwatumia wachezaji wake waliowaongeza katika dirisha dogo ambao ni Paul Kiongera, Brian Majwega, Novatus Lufungo na Hijja Ugando. 

Chanzo chetu cha habari kilisema Danny Lyanga yuko huru kucheza kwavile yeye tayari alikuwa amepitishwa, alichokuwa akisubiri ni ITC tu.

Post a Comment

 
Top