BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
BEKI wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa bado ana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na hajaona mchezaji wa kumkalisha benchi kama wengi wanavyofikiria.

Hivi karibuni wadau wengi wa soka wamekuwa wakidai kuwa kiwango cha Canavaro kimeanza kushuka na hivyo atafutiwe mbadala jambo ambalo yeye amesema kuwa wanaowaza hivyo wasahau kwani nafasi yake bado ipo kwenye kikosi hicho.


Yanga ilimsajili Cannavaro zaidi ya miaka 10 sasa na wamemleta beki, Mmali Vincent Bossou ili kumpa changamoto lakini bado Bossou hajafanikiwa na amekuwa mchezaji wa kukaa benchi.

Canavaro amesema kuwa anafahamu jinsi wadau wa soka wanavyomwangalia na kumfuatilia kwa sasa lakini bado anaamini uwezo wake ni mkubwa na si wa kukaa benchi kwasasa mpaka hapo baadaye sana.

"Katika soka kuna mambo mengi yanaweza kukutokea ama ukakumbana nayo, nafahamu jinsi watu wanavyofuatilia nyendo zangu kwa ukaribu lakini nataka kuwaambia kuwa wanaosubiri mimi niondolewe kikosi cha kwanza watasubiri sana na labda niamua mwenyewe kuondoka,'' alisema Canavaro

Canavaro ameweka wazi kuwa katika soka mchezaji ni lazima anaweza kuchemka katika baadhi ya mechi na hiyo inatokana na jinsi mchezaji anavyotumiwa ama ikitokea mchezaji ameumwa ndipo analazimika kukaa benchi.

"Kwenye kiksoi chetu kuna ushindani lakini binafsi sijaona mchezaji ambaye anaweza kunipoteza na kuchukuwa namba yangu, najiamini na ninaweza,'' alisema Canavaro

Canavaro ambaye ni nahodha wa Yanga na Taifa Stars amekuwa akichezeshwa mechi nyingi jambo ambalo limewafanya mashabiki wa soka kuanza kuona kama mchezaji ambaye kiwango chake kimeanza kushuka kwa kile kinachoelezwa anacheza chini ya kiwango.

Post a Comment

 
Top