BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi 'Mido', Mwanza
KOCHA msaidizi wa zamani wa Simba, Seleman Matola, jana aliiongoza timu yake mpya ya Geita Gold Mine kuifunga Simba mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana mjini Geita.

Matola aliondoka Simba kwa madai kuwa ameshindwa kufanya kazi na kocha mkuu Dylan Kerr kwavile hashauriki. Wawili hao waliingia kwenye sintofahamu hiyo mara baada ya timu kwenda kwenye mapumziko ya ligi.


Tangu hapo, Matola na Kerr hawakuwahi kuonekana tena wakiwa pamoja hadi jana kamera ya BOIPLUS ilipowanasa wakipeana 'hi'.

Licha ya kusalimiana na Kerr, Matola alionyesha kuzungumza kwa furaha na wachezaji kadhaa wakiwemo Peter Manyika Jr, Awadh Juma na Mohamed Fakih.

 Matola akiwa na Awadh Juma


 Hapa akakutana na Manyika Jr.


Hapa uso kwa uso na Kerr......Matola akiwa amepozi katika benchi la ufundi la Geita


Post a Comment

 
Top