BOIPLUS SPORTS BLOG

CHELSEA leo imeanza maisha bila  Jose Mourinho kwa kuanza kwa ushindi wa magoli  3-1 dhidi ya  Sunderland katika uwanja wa Stamford Bridge.

Guus Hiddink ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa muda mpaka mwishoni mwa msimu alikuwepo uwanjani lakini alitizama mechi hiyo akiwa jukwaani wakati  makocha  Steve Holland na  Eddie Newton ndio walioiongoza timu siku ya Leo.Mashabiki wa chelsea leo walionyesha sapoti kubwa kwa Mourinho, ambaye aliiwezesha timu hiyo kushinda makombe matatu ya ligi katika kipindi ambacho aliwahi kuifundisha timu hiyo. Mabango  kutoka kwa mashabiki wa Chelsea ya kumsifu Jose yalionekana uwanjani huku  Cesc Fabregas na Diego Costa majina yao yalizomewa wakati yalipotajwa Leo uwanjani.

  Branislav Ivanovic alianza kuifungia Chelsea goli la kwanza dakika tano baada ya mchezo huku Pedro nae alifunga goli lake la kwanza toka  Agosti na kuifanya Chelsea iongoze 2-0 baada ya  dk 13 za mchezo.


Oscar aliiongezea Chelsea goli la tatu kwa njia ya penati na kuifanya chelsea kuwa mbele kwa goli 3-0 kabla ya mchezaji wa zamani wa Chelsea Fabio Borini kuwafungia Sunderland goli la kufutia machozi.

Chelsea walifanya mabadiliko mawili kutoka kwenye mchezo wao wa jumatatu waliopoteza kwa  Leicester, ambapo Fabregas na Pedro walianza kwa Ramires na Eden Hazard,aliyeshindwa kucheza kutokana na kuwa majeruhi.


Post a Comment

 
Top