BOIPLUS SPORTS BLOG

Nairobi, Kenya
KOCHA wa Bayern Munich, Mhispania Pep Guardiola amewasili nchini Kenya kwa safari binafsi ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya utalii.

Guardiola alitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA) jana akiwa ameongozana na mkewe Cristina Serra, na watoto wao Maria Guardiola, Marius Guardiola na Valentina Guardiola.

Guardiola kulia akiwa na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho

Baada ya kuwasili, kocha huyu anayeheshimika sana barani Ulaya alijipiga picha 'selfie' na mashabiki wake raia wa Kenya ikiwa ni pamoja na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Joho alisema Guardiola efurahi kufika nchini Kenya na atakuwepo hadi mwaka mpya.

"Amefurahi sana kufika Kenya, atakuwepo hadi baada ya mwaka mpya ila amesema atahitaji utulivu kwa ajili kupumzika na familia yake". Alisema Joho.

Gavana Joho amemwalika kocha huyo anayeondoka Bayern kutembelea fukwe maridhawa za Mombasa. 

Baada tu ya kuwasili kwa ndege ya Emirates akitokea Dubai, Guardiola alikwenda moja kwa moja Masai Mara

Post a Comment

 
Top