BOIPLUS SPORTS BLOG

ALIYEKUWA meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu.
Ameteuliwa baada ya Jose Mourinho kufutwa Alhamisi.


"Nimefurahia kurejea Stamford Bridge. Chelsea ni moja ya klabu kubwa duniani lakini haimo pale inakofaa kuwa kwa sasa. Hata hivyo nina uhakika tunaweza kubadilisha mambo,” amesema Hiddink baada ya kuteuliwa. “Nasubiri kwa hamu kufanya kazi na wachezaji na wakufunzi wenzangu wapya katika klabu hii kubwa na kufufua uhusiano wangu mzuri na mashabiki wa Chelsea.”


Mholanzi huyo atakuwa uwanjani Stamford Bridge kutazama mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Sunderland lakini Steve Holland ndiye atakayesimamia mechi hiyo akisaidiwa na Eddie Newton, ambaye sasa atakuwa kocha msaidizi wa timu, klabu ya Chelsea imesema.

Hiddink, aliwahi kuinoa Chelsea wakati mmoja, alipowasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hajatia saini mkataba.

Post a Comment

 
Top