BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MATUMAINI ya Timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' kutetea ubingwa wa Kombe la Chalenji yalizimwa baada ya kufungashiwa virago na Rwanda kwa mikwaju ya penati kwenye mchezo uliochezwa leo jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Picha kwa hisani ya Futaa.com

Kenya na Rwanda zote zilipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao katika vipindi vyote viwili viwili, hivyo kupelekea kumaliza dakika 90 za mchezo kwa sare tasa.

Kutokana na suluhu hiyo mechi iliingia katika mikwaju ya penati ambapo Rwanda walifanikiwa kufunga penati zote tano zilizopigwa na Haruna Niyonzima, Jacques Tuyisenge,Djihad Bizimana, Isaiah Songa na Celestine Ndayishimiye, huku Kenya wakifunga penati tatu ambazo zilipigwa na Noah Abich,David Owino na Jesse Were

Kenya waliingia hatua ya robo fainali baada ya Uganda kuifunga Burundi mabao 2-0 kwavile wao walikuwa wameshapoteza mchezo wao dhidi ya Zanzibar kwa mabao 3-1.

Post a Comment

 
Top