BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
KIKOSI cha JKT Ruvu ya Pwani kimeipigisha kwata kikosi cha wanajeshi wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons kwa kuwafunga mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, jijini Dar es SalaamBeki Michael Aidan aliifungia JKT Ruvu mabao mawili kwa mipira ya adhabu ndogo katika dakika ya 10 na 33, mabao hayo yalitokana na timu hiyo kutawala sehemu kubwa ya mchezo katika kipindi hicho cha kwanza.

JKT Ruvu inayofundishwa na Abdallah Kibadeni iliendelea kuliandama lango la Prisons huku Aidan akionyesha uwezo mkubwa na kuwa nyota wa mchezo huo. Mashambulizi hayo yalizaa matunda dakika ya 35 ambapo Mussa Juma aliipatia timu yake bao la tatu.Dakika ya 37 Prisons walijipatia bao pekee la kufutia machozi kupitia kwa Mohamed Mkopi.

Kipindi cha pili kilishuhudia Samwel Kamuntu akiipatia JKT Ruvu bao la nne na kuwafanya JKT kuwa vinara wa mchezo huo kwa mabao 4-1.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, kati ya African Sports na Coastal Union 'Tanga Derby' timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1. Bao la Coastal lilifungwa na Juma Awadh huku lile la African Sports likifungwa na Mohamed Mtindi.

Post a Comment

 
Top