BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa Simba, Raphael Kiongera ambaye amejiunga jana na kikosi hicho kilichopo Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara amesema mechi yao ijayo dhidi ya Azam FC si ya kuibeza kwani ni ngumu.


Ugumu wa mechi hiyo inatokana na jinsi kikosi cha Azam kilivyo imara na kimekaa pamoja kwa muda mrefu na kusisitiza kuwa juhudi za pamoja zinaweza kuiangusha Azam katika mechi hiyo itakayochezwa Desemba 12, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kiongera ambaye alikuwa akiichezea KCB ya Kenya kwa mkopo ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha Simba leo asubuhi huku mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wakionyesha kufurahia ujio wake.

''Nimelipwa fedha zangu ndiyo maana nimekuja, nafurahi kwa hilo sidhani kama Simba wamenirudisha kwa ajili ya mechi ya Azam pekee, mechi hiyo itakuwa ngumu lakini tutashinda ingawa matokeo ni dakika 90 za mchezo, kikubwa ni ushirikiano kwa wote,'' alisema Kiongera

Kurejea kwa Kiongera kunaongeza ari na morali ndani ya Simba ambayo inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 huku Azam wakiwa kileleni kwa pointi 25, Yanga wana pointi 23 wakati Mtibwa Sugar wao wana pointi 22.

Post a Comment

 
Top