BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
MABINGWA wa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakutana na timu ya Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan katika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu hapo Jumapili.


Washindi wa ligi ya Japan, Hiroshima wamewalaza mabingwa wa Oceania, Auckland City mabao 2-0 leo kwenye mechi iliyochezewa Yokohama.

Mshindi wa mechi kati ya Mazembe na Hiroshima atakutana na mabingwa wa Amerika Kusini River Plate ya Argentina lwenye mchezo wa nusu fainali hapo Disemba 16.

Post a Comment

 
Top