BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MICHEZO ya Kombe la Shirikisho nchini (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili unatarajiwa kuanzia Disemba 15, ambapo timu 32 zitachuana kusaka nafasi ya kuingia mzunguko wa tatu wa kombe hilo.


Mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba, jumla ya timu 32 zilichuana kutoka Ligi Daraja la Pili, na timu 16 kusonga mbele hatua ya pili inayozikutanisha timu za Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) 16 na kufanya idadi ya timu 32 zinazosaka kufuzu kwa hatua ya mzunguko wa tatu.

Timu zilizofuzu kwa mzunguko wa pili kutoka mzunguko wa awali ni Abajalo FC, Mshikamano FC, Green Warriors, Villa Squad (Dar), Mvuvuma FC (Kigoma), Madini FC (Arusha), Sabasaba FC (Morogoro), Alliance, Pamba FC (Mwanza), Mighty Elephant (Songea), Kariakoo FC (Lindi), Wenda (Mbeya), Singida United (Singida).

Timu za Daraja la Kwanza zinaoanza kucheza mzunguko wa pili ni Polisi Tabora, Rhino Rangers, Burkinafaso, Friends Rangers, KMC, African Lyon, Ashanti United, JKT Oljoro, Panone FC, Kiluvya United, Lipuli FC, Kurugenzi, Mbao FC, Geita Gold, JKT Mlale, Njombe Mji, Kimondo, Mji Mkuu na JKT Kanembwa.

Post a Comment

 
Top