BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi amenunua gari aina ya Toyota Landcruiser lenye thamani ya dola 23,500 sawa na Sh 47 milioni.


Tambwe atakuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Yanga kumiliki gari lenye thamani hiyo katika wachezaji wote waliopo kwenye kikosi hicho wanaomiliki magari ya kifahari.

Tambwe ameiambia BOIPLUS kuwa gari hilo aliliagiza nchini Japan ambapo ilipita Bandari ya Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda Burundi kwa ajili ya kulisajili.


Alisema kuwa gharama za ununuzi na saufirishaji kutoka Japan mpaka Dar es Salaam ni dola 14,000, kusafirisha kwenda Burundi ni dola 2,000 wakati ushuru alilipa dola 7,500.

''Ni mali yangu kweli, hili gari niliagiza Japan na ni ndoto ambazo nilikuwa nazo toka mwanzo ila nilisubiri kujipanga kwanza,'' alisema Tambwe.


Post a Comment

 
Top