BOIPLUS SPORTS BLOG

LEICESTER City wamerudi kileleni baaada ya kuifunga timu ya Chelsea kwa mabao 2-1 wakiwaacha mabingwa hao  watetezi wakiwa wameduwaaa.


Jamie Vardy  na Riyad Mahrez vijana wa Claudio Ranieri ndio waliopeleka kilio kwa The blues, ambao wote walifunga na kuwafanya wafikishe jumla ya magoli 26.

Alikuwa ni vardy aliyeanza kupeleka kilio kwa Chelsea baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Mahrez bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.

 Dakika ya 48 mpishi wa bao la kwanza Mahrez aliwainua vitini mashabiki wa Leicester City kwa kufunga bao zuri lililomwacha golikipa wa chelsea akiruka bila mafanikio.


 Loic Remy aliifungia chelsea bao  katika dk ya 77 hali  iliyowapa hamasa ya kuendelea kulisakama lango La Leicester City bila mafanikio na hivyo  hadi mwisho wa mchezo vijana hao wa Ranieri kocha wa zamani wa Chelsea kuibuka na ushindi.

Ranieri alianza na kikosi kile kile  ambacho kilipata ushindi wa goli 3-0 dhid ya swansea City. 


  Vikosi vilivyoanza ni Kama ifuatavyo.

Leicester City XI:
Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Drinkwater, Kante, Albrighton; Ulloa, Vardy.

Substitutes: Schwarzer, Benalouane, Wasilewski, Inler, King, Dyer, Okazaki​

Chelsea XI: 
Courtois, Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Oscar, Hazard; Diego Costa

Substitutes: Begovic, Cahill, Mikel, Fabregas, Kenedy, Pedro, Remy.

Post a Comment

 
Top