BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
LICHA ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya  Cadiz, Real Madrid wanaweza kutolewa kwenye mashindani ya kombe la mfalme kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakupaswa kucheza kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.


Winger Denis Cheryshev mwenye asili ya Russia alianza mchezo huu wa raundi ya nne ugenini dhidi ya timu ya Cadiz japokuwa alikuwa ana adhabu ya kutumikia baada ya kuwa na kadi tatu za njano, ya mwisho akiipata katika mchezo wa nusu fainal ya msimu uliopita.


Cheryshev alikuwa kwa mkopo katika club ya Villareal wakati anapewa kadi ya tatu ya njano katika kipigo cha 3-1 dhid ya Barcelona mwezi machi na adhabu ilikuwa inaendelea kwenye mashindano yanayofwata.

Mchambuzi maarufu wa kituo cha Sky Sports Spain,   Guillem Balague aliiambia 
Sky Sports News HQ kwamba  Denis Cheryshev alijumuishwa kwenye kikosi ambacho kilicheza mechi dhid ya Cadiz.


"Lakini  Cheryshev alipewa kadi ya tatu ya njano katika mchezo wa pili wa nusu fainal msimu uliopita wakati yupo kwa mkopo Villareal dhidi ya Barcelona.


Real Madrid walishinda mchezo wao huo wa kombe la mfalme  ugenini lakini wana hati hati ya kuondolewa mashindanoni.


Baada ya dakika takribani mbili ama tatu Radio ya Spain ilitoa habari hii kwamba hakustahili kucheza hali iliyosababisha mashabiki wa Cadiz kujawa na furaha na kuanza kusema  Benitez angalia kwenye mtandao wa twitter wakimaanisha kwamba Madrid watondolewa mashindanoni.

Tukio Kama hili liliwahi kuwatokea osasuna mwezi septemba kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakustahili na aliindolewa mashindanoni.

Post a Comment

 
Top