BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
TIMU ya Liverpool imekua timu ya mwisho kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi maarufu kama Capital one .Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuichapa timu ya Southampton kichapo cha mabao 6-1.

Southampton walianza kuandika bao la mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Sadio Mane.

Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia mshambuliaji wao Daniel Sturridge katika dakika ya katika dakika ya 29 , Sturridge, tena akaongeaza bao la pili.

Mshambuliaji Divock Origi akaongeza mabao mengine matatu katika dakika ya 45, 68, 86, huku Jordan Ibe nae akifunga bao moja, na kukamilisha idadi ya mabao 6.Michezo ya nusu fainali ya kwanza itafanyika January 5 na 6 na michezo ya marudio ikifanyika 25 na 26 ambapo Liverpool watachuana na Stoke City katika mchezo wa nusu fainali huku Manchester City wao wakikabiliana na Everton

Post a Comment

 
Top