BOIPLUS SPORTS BLOG

Manchester, Uingereza
MANCHESTER City ipo kwenye mchakato wa kubadili nembo yake na ilipanga kuitambulisha nembo mpya siku ya Desemba 26 'Boxing Day' kama zawadi maalumu kwa mashabiki wake. Unajua kilichotokea? Nembo imesambaa mtaani siku tatu kabla.Kushoto, nembo ya zamani wakati kulia ni mpya iliyovuja


Nembo hiyo imeonekana kwenye tovuti ya ofisi ya serikali inayohusika na usajili wa nembo huku uongozi wa Man City ukiwa umebandika mabango mtaani kuelezea uzinduzi wake na jinsi itakavyokuwa ikionekana.

Katika nembo mpya hakuna picha ya tai wa rangi ya dhahabu, nyota na 'motto' ya klabu huku sasa  ikibadilishwa na kuwa ya duara na nyongeza ya ua jekundu la Rose, neno City na mwaka 1894 ambao ndio klabu ilianzishwa.


Kutoka kushoto ni nembo zilizotumika kuanzia 1930 hadi 2015


Mashabiki wengi wametoa maoni yao kuwa mabadiliko yamekuwa makubwa sana kiasi vitu vya msingi vimeondolewa. Lakini kuna baadhi wamepongeza kwavile logo hiyo imefanana na ile iliyotumika kuanzia mwaka 1972 hadi 1997.

Badiliko linalopigiwa kelele zaidi ni kuondolewa kwa neno FC 'Football Club', jambo hili liliwahi pia kufanywa na majirani zao Manchester United mwaka 1998 nao walipoliondoa neno FC.

Post a Comment

 
Top