BOIPLUS SPORTS BLOGRAHEEM Sterling amefunga mara mbili na kuchagiza ushindi wa bao 4-2 wa Manchester City dhidi ya Borussia M'gladbach na kuongoza kundi D.

Kwa kushika nafasi ya kwanza, City inafanikiwa kuvikwepa vigogo kama Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa. Juventus iliyochapwa 1-0 na Sevilla, imeshika nafasi ya pili kundi D.

Hadi dakika ya 79, City ilikuwa nyuma kwa bao 2-1, lakini magoli ya haraka haraka kupitia kwa Sterling aliyefunga mara mbili na Wilfried Bony, yakaipa ushindi mnono Manchester City.

Man City: Hart 6, Clichy 5.5 (Sagna 80), Otamendi 6, Mangala 6, Kolarov 5.5, De Bruyne 6 (Navas 65, 6.5), Delph 6 (Bony 65, 7.5), Fernandinho 6, Silva 7, Toure 7, Sterling 8.5.
Wafungaji: Silva 16, Sterling 79, 81, Bony 85.

Borussia M'gladbach: Sommer 6, Elvedi 5.5, Christensen 5.5, Nordtveit 6, Wendt 6 (Hazard 84), Korb 7.5, Dahoud 6 (Schulz 66, 6), Xhaka 6.5, Johnson 7 (Drmic 72, 6), Stindl 6.5, Raffael 7.
Wafungaji: Korb 18, Raffael 42

Post a Comment

 
Top