BOIPLUS SPORTS BLOG

WILFRED Bony amefunga bao moja dakika ya 26 dhidi ya timu yake ya zamani Swansea City na kuchangia kuipa Manchester City pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.


Katika mchezo huo uliochezwa Etihad Stadium, City imevuna kwa mbinde ushindi wa bao 2-1 huku Swansea ikijilaumu yenye kupoteza mechi hiyo baada ya kusawazisha dakika ya 90.


Bafetimbi Gomis aliifungia bao Swansea ambalo lingewafanya waambulie pointi moja, lakini kabla hawajamaliza furaha yao, Yaya Toure akaifungia Manchester City ndani ya dakika tatu za majeruhi.
Ushindi huo umeifanya Manchester City irejee kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi 32 na kuishusha Leicester City kwa tofauti ya magoli.

Leicester City ambayo nayo ina pointi 32 itakuwa na kibarua cha kusaka tena nafasi ya kwanza wakati itakapomenyana na Chelsea Jumatatu usiku.


Arsenal yenye pointi 30 nayo itakuwa na nafasi nzuri ya kuongoza ligi iwapo itainyuka Aston Villa Jumapili jioni.

Matokeo mengine ni Kama yafutavyo:
FT Norwich City 1 - 1 Everton
FT Crystal Palace 1 - 0 Southampton
FT West Ham United 0 - 0 Stoke City
FT Manchester City 2 - 1 Swansea City
FT Sunderland 0 - 1 Watford
FT AFC Bournemouth 2 - 1 Manchester United

Post a Comment

 
Top