BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
 MASHABIKI wa Manchester United wanaendelea kuumuka kwa hasira kufuatia soka bovu linaloendelea kuonyeshwa na timu hiyo chini ya kocha Louis van Gaal.Kwa mara nyingine tena, United imetandaza soka la mashaka matupu kwenye mchezo wa Premier League dhidi ya West Ham na kujikuta ikiambulia sare tasa katika uwanja wao wa nyumbani, Old Trafford.

Katika michezo sita ya mwisho ndani ya Old Trafford, United imetoka sare ya bila magoli mara nne, hali inayopelekea mashabiki wa klabu hiyo wachanganyikiwe na kupiga makelele ya kutaka timu icheze kwa kushambulia - ‘attack, attack, attack’ (shambulia, shambulia, shambulia).Katika kuonyesha namna walivyokerwa, baadhi ya mashabiki wa Machester United waliojazana Old Trafford, walianza kutoka nje ya uwanja hata kabla mchezo haujaisha.

West Ham ndiyo iliyoonekana iliingia uwanjani kusaka ushindi, ikacheza soka la kushambulia na kugonga nguzo mara mbili.

Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6.5; McNair 6.5 (Varela 46, 6), Smalling 6, Blind 5.5, Darmian 6; Schweinsteiger 6 (Depay 73, 7), Schneiderlin 5.5 (Carrick 44, 6); Mata 5.5, Fellaini 6.5, Lingard 6.5; Martial 6.5.

West Ham (4-2-3-1): Adrian 7; Tomkins 6.5, Reid 8, Ogbonna 6, Cresswell 6.5; Song 6.5 (Obiang 77, 6), Kouyate 6.5; Moses 5.5 (Antonio 37, 6), Noble 6, Zarate 6 (Jenkinson 87); Carroll 7.Wakati huo huo, Klabu ya Manchester City imepoteza nafasi yakuendelea kuongoza Ligi ya EPL baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Stoke City, ambapo mabao yote yalipatikana kipindi cha kwanza katika dakika ya 7 na 15 kupitia kwa Marko Arnautovic.

Post a Comment

 
Top