BOIPLUS SPORTS BLOG

TIMU za Sevilla, Espanyol, Real Betis na  Deportivo La Coruna zote zimesonga mbele kuingia hatua ya 16 bora ya  Copa Del Rey (kombe la mfalme) siku ya jumanne na kuungana na Barcelona  na Cadiz ambao wao wamekwishafuzu.


Deportivo wao walitoka sare ya 1-1 na timu ya daraja LA pili Llagostera katika mzunguko wa nne, na wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 3-2.

Real Betis, 2-0 walishinda nyumbani ambapo Jana walitoka nyuma 3-1 na kupata suluhu ya 3-3 na hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-3


Sevilla wao walikuwa tayari wameshatia mguu mmoja ndani ya 16  baada ya ushindi wa 3-0 ugenini na katika mechi ya marudiano katika uwanja wao wa nyumbani Jana walishinda 2-0 dhid ya Logrones.

Espanyol, wao nao wameanza na mwanzo mzuri na kocha wao mpya raia wa romania Constantin Galca, baada ya kutoka nyuma ya  goli 1 na kwenda kushinda  2-1, hivyo kusonga kwa jumla ya mabao 3-2.


Mabingwa watetezi wao tayari wamejihakikishia nafasi yao hatua ya 16  baada ya ushindi wa goli  6-1 dhid ya Villanovense.

Real Madrid waliondolewa mashindanoni baada ya kumchezesha mchezaji aliyekuwa anatumikia adhabu dhidi ya  Cadiz, hii imewapa timu ya daraja LA tatu kusonga mbele.

 Gary Neville Leo atakuwa na nafasi nzuri ya kupata ushindi wake wa kwanza Kama kocha wa valencia watakaposhuka dimban leo the Mestalla.Valencia tayari mechi ya kwanza waliwafunga  Basques 3-1 kabla ya  Neville hajateuliwa kuwa kocha mpya.

Post a Comment

 
Top