BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Ally Shatry 'Chico'
TIMU ya soka ya Geita Gold Mine leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Wajja Spring school mjini Geita. Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 32 mfungaji akiwa ni Brian Majwega kabla Pastory Kaisi hajaisawazishia Geita kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 44. Penati hiyo ilitokana na kipa wa Simba Peter Manyika Jr kumfanyia madhambi mshambuliaji huyo. 

Katika dakika ya 62 ,Geita inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Selemani Matola, ilipata bao la pili kupitia kwa Juvenile Pastory huku bao la tatu likifungwa na Emmanuel Swita katika dakika ya 84 kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Simba sc Emery nimubona kushika mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi Athony Mpalila kuamuru ipigwe penati.Simba imerejea jijini Mwanza ambako inaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mwadui mchezo utakaopigwa siku ya jumamosi mjini Shinyanga.

Post a Comment

 
Top