BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
RAIS wa Jamhuri ya Muungano, John Pombe Magufuli leo ametangaza mawaziri 19 huku Wizara zingine hazitakuwa na manaibu waziri na kumteua Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.Magufuli ameunda Baraza dogo la mawaziri lengo kubwa ni kupunguza gharama ambapo kiasi cha Sh 2 bilioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri hao ametaka zitumike kufanya shughuli nyingine ikiwemo ununuzi wa madawati na utoaji wa elimu bure.

Katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Dr Jakaya Kikwete, Wizara hiyo ya Habari ilikuwa ikiongozwa na Mheshimiwa Fenella Mkangara na sasa itakuwa chini ya Nnauye aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Mbunge wa Mtama.

Mawaziri wengine waliotangazwa leo ni Ofisi ya Rais, Tamisemi Utumishi na Utawala bora itakuwa chini ya  George Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu Waziri ni Jaffo Suleiman Said.

Wizara ya Mazingira itaongozwa na Januari Makamba na hana msaidizi, Wizara ya Ajira na Walemavu ni Jenista Mhagama, Naibu wake ni mbunge, Pos Abdallah ambaye ni mhadhiri Chuo kikuu cha Dodoma.

Wizara ya Walemavu, Waziri wake ni Anthony Mavunde, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi itakuwa chini ya Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu ni Willium Tate Olenasha.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano bado haijatafutiwa Waziri kwani anaendelea kufikiriwa  ila Naibu Waziri wake ni Eng Edwin Amandus Ngonyani huku Wizara ya Fedha na Mipango pia haijapata Waziri lakini Naibu wake ni Dr. Ashantu Kijaji.

Wizara ya Nishati na Madini, Waziri ni Sospeter Muhongo naibu wake ni Dr. Medard Kalemani huku Wizara ya Katiba na Sheria ipo chini ya Dr. Harrison Mwakyembe. Wizara ya 
Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Augustino Mahiga, naibu waziri ni Dr Suzan Kolimba

Wizara ya Ulinzi na kujenga taifa: Waziri Dr. Hussein Mwinyi. Wizara ya 
Ardhi na maendeleo ya makazi Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu wake ni Angelina Mabula. Wizara ya Utalii bado haijafanyiwa kazi lakini naibu ni Eng Ramo Makani wakati Wizara ya Viwanda na Biashara Waziri ni  Charles Mwijage.

Wizara ya Sayansi na Ufundi, Naibu ni Eng. Stella Manyanya, Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Waziri ni Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala wakati Wizara ya maji na umwagiliaji ni Makame Mbarawa, Naibu wake ni Eng Isack Kamwela.

Rais Magufuli bado anaendelea kufanyia kazi wizara ambazo hazijapata mawaziri ambapo atatangaza mara tu ya kukamilisha mchakato huo.

Post a Comment

 
Top