BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
TP Mazembe leo inaanza mashindano ya kusaka klabu bingwa dunia kwa kuwavaa mabingwa wa Japan, Sanfrecce Hiroshima, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Nagai jijini Osaka.

Mechi hiyo ya robo fainali itakayotoa timu itakayopambana na River Plate katika nusu Fainali itaanza majira ya saa 7:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.


Akizungumza na BOIPLUS kwa njia ya simu kutoka Japan, mshambuliaji wa kutumainiwa wa Mazembe, mtanzania Mbwana Samatta alikiri kuwa mechi ni ngumu kwavile wanapambana na mabingwa ambao pia wanacheza nyumbani kwao, ila wana uhakika wa kuibuka na ushindi na kuliwakilisha vema bara la Afrika.

"Jamaa ni mabingwa wa hapa na si unajua wanacheza kwao bwana, ila tumejiandaa vizuri, mechi itakuwa ngumu ila Mungu atajalia tutawatoa tu."

Mechi nyingine ya mapema itawakutanisha Club America na Guangzhou Evergrande mechi itakayopigwa majira ya saa 4:00 asubuhi hii katika uwanja huo huo wa Nagai.

BOIPLUS inawatakia kila la heri watanzania Samatta na Thomas Ulimwengu pamoja na timu yao ya Mazembe.

Post a Comment

 
Top