BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MABINGWA wa Afrika TP Mazembe, leo wameshindwa kukamata japo nafasi ya tano kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu za Soka baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Club America ya Mexico.


Katika mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Nagai jijini Osaka, Club America ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Mazembe kwa bao safi la straika Dario Benedetto katika dakika ya 19.

Dakika 9 baadae, America ilijipatia bao la pili na safari hii mfungaji akiwa ni Martin Zuniga kabla Rainford Kalaba hajaipatia Mazembe bao la kufutia machozi katika dakika ya 43.


Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini America ndio ambao walitawala zaidi mchezo huku ikishuhudiwa Mtanzania anayeichezea Mazembe, Mbwana Samatta akipiga mashuti mengi zaidi (8) langoni sawa na straika wa America, Michael Aroyo.


Hadi mwamuzi Alireza Faghani kutoka Iran anapuliza kipenga cha kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, Club America iliibuka kidedea kwa ushindi huo wa mabao 2-1

Post a Comment

 
Top