BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude amesema anaumizwa na matokeo mabovu ya Simba ambayo wamekuwa wakiyapata kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bata.


Akizungumza na BOIPLUS kiungo huyo alisema kuwa wao kama wachezaji wanapambana kuhakikisha wanapata ushindi na kulalamikia kuwa waamuzi ndio wanaowaumiza zaidi katika kutoa uamuzi wao.

Mkude alisema kuwa Ligi Kuu Bara kwasasa ni ngumu hivyo viongozi pamoja na wanachama wake wanatakiwa kuwa karibu na timu yao ili kuwapa sapoti.


''Mengi yanatokea kwasasa ambayo ni kama changamoto tu kwangu, kikubwa tunatakiwa kupewa ushirikiano wa kutosha kwani ukiangalia sisi kama wachezaji tunapambana vya kutosha ili timu ishinde, ligi imekuwa ngumu na waamuzi hawatoi uamuzi ulio sahihi,'' alisema Mkude na kuongeza

''Wengine wanasema mimi ni mlevi sana. Inafikia kipindi nashindwa hata kutoka na rafiki zangu sasa hivi kwasababu ukionekana tu basi taarifa zinasambaa isivyo basi wanalinganisha na matokeo mabaya ya timu inakuwa tatizo zaidi,'' alisema

Post a Comment

 
Top