BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
BAADA ya matokeo kadhaa mabaya yaliyotishia uhai wa kibarua cha Jose Mourinho, hatimaye upepo umegeuka na angalau kwa sasa kocha huyo yuko salama salmin baada ya kuivusha Chelsea kwenda hatua ya mtoano ya Champions League (16 bora).Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich, akiwa amekaa na mkewe Dasha Khukova kwenye uwanja wa Stamford Bridge, alishuhudia Chelsea ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Porto.

Ushindi huo dhidi ya Porto katika mchezo wa kundi G, ni kinga tosha kwa Mourinho lakini shukran zaidi kwake ziwandee Diego Costa na Willian.

Diego Costa alisababisha goli la kwanza dakika ya 12 baada ya mpira wake uliookolewa na kipa Iker Casillas kumgonga Ivan Marcano na kujaa wavuni huku Willian akitupia bao la pili dakika ya 52.Chelsea imeshika nafasi ya kwanza kundi G huku Dynamo Kyiv iliyoinyoa Maccabi Tel Aviv 1 - 0 ikikamata nafasi ya pili wakati Porto iliyokuwa ikiongoza kundi hilo kwa muda mrefu ikiangukia nafasi ya tatu na sasa itakwenda kucheza Europa League.

Chelsea (4-2-3-1): Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Ramires, Matic; Willian, Oscar (Pedro 80), Hazard (Remy 89); Diego Costa (Mikel 85)

Porto (4-3-3): Casillas; Maxi Pereira (Neves 57), Marcano Sierra, Maicon, Indi; Herrera (Tello 70), Danilo, Imbula (Aboubakar 56); Corona, Brahimi, Layun


Post a Comment

 
Top