BOIPLUS SPORTS BLOG

KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefukuzwa kazi baada ya klabu hiyo kupata matokeo mabaya mfululizo.

Chelsea ambao ni mabingwa wa Ligi kuu Uingereza msimu uliopita imekuwa katika kiwango kibovu msimu huu wakiwa pointi moja tu mstari wa eneo la kushushwa daraja.


Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatma ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 hadi kufikia sasa.

Mechi ya mwisho kwa Mourinho kukaa benchi ilikuwa Jumatatu walipochapwa na vinara wa ligi Leicester City 2-1.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.

Post a Comment

 
Top