BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA Mkuu wa Toto Africans, John Tegete amesema kuwa kufungwa na African Sports bao 1-0 kulichangiwa na maandalizi mabovu pamoja na kucheleweshewa chakula siku ya mechi iliyochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Toto ilipokea kipigo hicho ikiwa ni siku chache baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Simba kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja huo.

“Tumepoteza mechi kwasababu hatukujiandaa vizuri toka mwanzo, siku ya mechi wachezaji walilalamika  kupewa chakula saa tisa na nusu muda mfupi kabla ya mechi hiyo kuchezwa,” alisema Tegete na kuongeza

''Kinachonisikitisha ni kufungwa na timu ndogo tena ambayo haiko imara kwani kiuwezo haitufikii, lakini naamini mechi ijayo haya hayatatokea,'' alisema

Hivi karibuni wachezaji wa Toto walilalamikia ugumu wa maisha wanayokumbana nsyo kwenye timu hiyo ikiwemo ukata.

Post a Comment

 
Top