BOIPLUS SPORTS BLOG

MIEZI mitano tu toka Yanga isaini mkataba wa miaka miwili na Haruna Niyonzima, leo uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuvunja mkataba wake na kiungo huyo kutoka Rwanda.Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema Niyonzima atalazimika kulipa kiasi cha dola 71,175 ambayo ni zaidi ya Sh 149 milioni kwa kufanya mambo yaliyosababisha mkataba huo uvunjike.

Chanzo cha mgogoro huo ni kitendo cha Niyonzima kuchelewa kurudi Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Ethiopia. Hii ilipelekea uongozi kumsimamisha kwa muda usiojulikana wakati jambo lake likiendelea kujadiliwa.

Niyonzima amekuwa na tabia ya kuchelewa kurejea kazini kila anaposafiri kwenda kwao.
Post a Comment

 
Top