BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
STRAIKA mwenye nguvu aliyekuwa akikipiga na Mwadui Fc ya Shinyanga, Paul Nonga, leo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu ya Yanga ya jijini Dar Es Salaam.


Akizungumza na BOIPLUS mara baada ya kusaini mkataba huo Nonga anayesifika kwa uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu alikiri kukamilisha 'deal' hiyo na kwamba anajaribu kuzungumza na mabosi wake wapya wampe ruhusa ya kurejea Shinyanga kwa ajili kubeba vifaa vyake.

"Ni kweli nimesaini miaka miwili, hapa saizi nazungumza na viongozi wangu kama wanaweza kuniruhusu nirudi Shinyanga kubeba vitu vyangu, na hii ni kwavile nilikuja mimi tu bila chochote. Ila kama hawatakubali basi itabidi nisubiri tu kujiunga na timu". Alisema Nonga.

Kwa kutua Yanga, straika huyo wa zamani wa Mbeya City atakumbana na upinzani mkubwa wa namba kutoka kwa washambuliaji wa kati Amiss Tambwe, Donald Ngoma na Malimi Busungu huku timu hiyo ikiwa pia na viungo wa pembeni kama Simon Msuva, Deus Kaseke na kiungo mpya kutoka Niger Issoufou Boubacar 'Diego'  

Post a Comment

 
Top