BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MBEYA City kesho wanacheza na Mgambo Shooting na tayari Shirikisho la soka nchini (TFF) limeruhusu kuwatumia wachezaji wao wote waliowasajili ambao hawakuweza kucheza mechi yao ya awali dhidi ya Mtibwa Sugar.


Juma Kaseja

Katika usajili wa dirisha dogo Mbeya City, imewasajili wachezaji kadhaa wakiwemo Abdallah Juma, Ramadhan Chombo 'Redondo' ambao wanaungana na wenzao Haruna Moshi 'Boban', Juma Kaseja na Haruna Shamte ambao wote wamewahi kuichezea simba ya jijini Dar es Salaam.

Usajili huo umempa matumaini mapya kocha mkuu wa City, Meja Mstaafu Abdul  Mingange, ameweka wazi sababu za kuwasajili nyota hao wa zamani wa Simba kuwa wachezaji wanaotoka timu za kubwa kama Simba, Yanga na Azam, husaidia kuleta upinzani kwenye kikosi."Nilikuwa na kikosi kizuri lakini kilikuwa na vijana wengi, hivyo uwepo wa hawa wachezaji wazoefu kutasaidia kuleta ushindani kwenye kikosi changu, na kuleta utulivu hasa wanapokuwa na mechi kubwa hasa za Simba, Yanga na Azam, hawa wamepitia huko naamini watakuwa mwiba kwao na ushindani utaongezeka.

"Tunacheza na Mgambo ambayo imetoka sare na Yanga, hivyo haitakuwa mechi rahisi kwa pande zote mbili ila nawapanga wachezaji wangu wazoefu kuhakikisha tunafanya vizuri," alisema Mingange

Post a Comment

 
Top