BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa Gor Mahia, Michael Olunga jana Jumatano alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Kenya (KPL) katika sherehe za tuzo hizo zilizofanyika nchini humo.


Olunga ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wanawindwa na Simba tangu alipofanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Kagame iliyofanyika nchini mwezi Julai mwaka huu huku Azam ikutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Olunga amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 19 na kuisadia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa KPL. Kiungo, Khalid Aucho naye wa Gor Mahia aliyekuwa akiwaniwa na Yanga alishika nafasi ya pili katika tuzo ya kiungo bora wa msimu.


Kipa Boniface Oluoch ambaye alitakiwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa kutwaa tuzo ya kipa bora wa msimu.

Akizungumza mara baada ya tuzo hizo, Olunga alisema kuwa "Nafurahi kwa tuzo hii na inanifanya kuongeza bidii katika soka, nawashukuru wote pamoja na timu yangu ya Gor Mahia,".

Post a Comment

 
Top