BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
CRISTIANO Ronaldo ameweka rekodi mpya hatua ya makundi Champions League wakati Real Madrid ikiichapa Malmo bao 8-0.


Ronaldo akafunga mara nne na kufanikiwa kujikusanyia jumla ya mabao 11 hatua ya makundi ambayo ni rekodi mpya kwenye michuano hiyo.

Karim Benzema naye akafunga mara tatu huku bao lingine la Real Madrid likifungwa na Mateo Kovacic.


Hata kabla ya mchezo huo, Real Madrid ilishajihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi A, lakini hiyo haikuwa sababu ya kuacha kuingushia Malmo kipigo cha mbwa mwizi.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Paris Saint Germain iliyoshika nafasi ya pili, ikaichapa Shakhtar Donetsk 2 – 0 kwa magoli ya Lucas Moura na Zlatan Ibrahimovic.

Post a Comment

 
Top