BOIPLUS SPORTS BLOG

NAHODHA wa Manchester United anajiandaa kurejea mchezoni kwenye mechi dhidi ya Norwich siku ya jumamosi baada ya kupona majeraha ya enka yaliyomuweka nje  kwenye mechi za West Ham, Wolfsburg na  Bournemouth. Kama atacheza mechi hiyo atakuwa ametimiza jumla ya michezo 500 aliyoichezea Man United.Rooney alijiunga na Man United toka  Everton  mwaka 2004 kwa Ada ya paundi milioni 25.6 akiwa na miaka 18 na alifunga magoli matatu(hattrick) kwenye mchezo wake wa kwanza tu kwenye klabu Bingwa Ulaya  katika ushindi wa magoli 6-2 dhidi ya Fenerbahce.

Mshambuliaji huyo ameshinda mataji matano ya ligi, taji la klabu bingwa na pia ameahinda tuzo binafsi mbali mbali.
Hapa tunaangalia takwimu muhimu katika michezo 499 aliyoichezea man united katika mashindano mbali mbali.

Post a Comment

 
Top