BOIPLUS SPORTS BLOG

MSHAMBULIAJI hatari wa Taifa Stars ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu bora na shirikisho la soka la Afrika CAF wanaocheza soka barani Afrika.


Samatta anawania tuzo hiyo na wachezaji wengine wawili Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel pamoja na Kipa machachari wa TP Mazembe ya DR Congo Robert Kidiaba.

Mshindi atachaguliwa na makocha wa timu za taifa na kutangazwa katika dhifa maalum Januari 7 mwakani.

CAF ilikuwa imewataja wachezaji 37 katika orodha ya awali lakini wakachujwa hadi kufikia 10 mwezi uliopita.


Wakati huo huo ikiwa ni siku chache tu baada ya kutawazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na shirika la BBC, kiungo Yaya Toure ametajwa miongoni mwa wachezaji watatu bora kuwania taji la mchezaji bora wa mwaka huu na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Tuzo hii huwajumuisha wachezaji wa Afrika wanaocheza soka ng'ambo.
Nyota huyo wa Manchester City kwa mara nyingine atakuwa akipigania taji hilo dhidi ya mshambulizi wa Black Stars ya Ghana na Swansea Andre 'Dede' Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund.

Endapo atashinda kigogo huyo wa The Elephants ya Ivory Coast, atakuwa mtu wa kwanza kunyakua taji hilo kwa mara ya tano.

Toure, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mapema mwaka huu pamoja na aliyekuwa nahodha wa Cameroon Samuel Eto'o ndio wachezaji wa pekee waliowahi kutwaa taji la mchezaji bora wa Afrika mara 4.

Eto'o alitwaa taji hilo katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.
Wanaowania tuzo za 2015 ya CAF

Wanamichezo wengine walioingia fainali ni kama ifuatavyo;

Mchezaji bora mwanamke 2015:
Gabrielle Onguéné - Cameroon
Gaelle Enganamouit - Cameroon
Ngozi Ebere - Nigeria
N'rehy Tia Ines - Ivory Coast
Portia Boakye - Ghana

Chipukizi bora wa 2015:
Adama Traore - Mali
Kelechi Nwakali - Nigeria
Samuel Diarra - Mali
Victor Osimhen - Nigeria
Yaw Yeboah - Ghana

Anayeonesha matumaini:
Azubuike Okechukwu - Nigeria
Etebo Oghenekaro - Nigeria
Djigui Diarra - Mali
Mahmoud 'Kahraba' Abdelmonem - Misri
Zinedine Ferhat - Algeria

Kocha bora mwaka 2015:
Baye Ba - Mali U -17
Emmanuel Amunike - Nigeria U -17
Fawzi Benzarti - Etoile du Sahel
Hervé Renard - Ivory Coast
Patrice Carteron - TP Mazembe

Refarii bora mwaka 2015:
Alioum Neant - Cameroon
Bakary Papa Gassama - The Gambia
Eric Arnaud Otogo Castane - Gabon
Ghead Zaglol Grisha - Egypt
Janny Sikazwe - Zambia

Mwafrika aliyebobea:
CK Gyamfi - Ghana
Samuel Mbappé Léppé - Cameroon

Timu bora ya taifa :
Ivory Coast
Ghana
Mali U-17
Nigeria U-17
Nigeria U-23

Timu bora ya taifa ya wanawake:
Ghana,
Cameroon,
Afrika Kusini,
Zimbabwe

Klabu bora 2015:
USM Algers - Algeria
TP Mazembe - DR Congo
Orlando Pirates - Afrika Kusini
Etoile du Sahel - Tunisia

Post a Comment

 
Top