BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MBEYA City leo imeendelea kupata matokeo ya sare kwenye Uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare na Magambo JKT kwa bao 1-1. Mechi hiyo imepigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Azam FC ikiifunga Majimaji Fc bao 2-1.


Azam wamepata ushindi huo wa ugenini na kufikisha pointi 29 nyuma ya Yanga ambao wana pointi 30. Mabao ya Azam yalifungwa na Didier Kavumbagu pamoja na Ame Ally Zungu katika dakika za 10 na 20 wakati bao la Majimaji lilifungwa na Alex Kondo katika dakika ya 58.

City na Mgambo ziliingia uwanjani huku zote zikiwa na kumbukumbu ya matokeo ya sare katika mechi zilizopita ambapo Mgambo ilicheza na  Yanga wakati City walicheza na Mtibwa Sugar.


Mbeya City ndiyo ilikuwa ya kwanza kucheka na nyavu za wapinzani wao kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Abdallah Juma baada ya kuunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Hassan Mwasapili.

Azizi Gilla wa Mgambo aliisawazishia timu yake bao ikiwa ni dakika ya 75 mpira ambao ulikuwa ni wa piga nikupige katika lango la Mbeya City.

Katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, JKT Ruvu ilitoka sare ya bao 2-2 na Coastal Union.

Post a Comment

 
Top