BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
TAWI la Simba lililopo Kimara Temboni maarufu kama Simba Dume leo wamefanya uchaguzi wao ambao umewaweka madarakani viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa Katiba yao pamoja na ile ya Klabu ya Simba.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Katibu wa Matawi ya Simba Wilaya ya Kinondoni, Ally Mkande ambapo wanachama 36 ndiyo waliopiga kura kati ya wanachama 72 wa tawi hilo.

Mwenyekiti, Benny Shija


Mwenyekiti wa zamani wa tawi hilo, Ben Shija alifanikiwa kutetea kiti hicho kwani hakuwa na mpinzani ambapo kati ya kura 36 zilizopigwa alipata kura 35. 

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Daniel Mangesho aliyepata kura 32 aliyewapiku wapinzani wake wawili Josephag Shilugile na Charles Mwkaingili waliopata kura mbili kila mmoja.


Nafasi za wajumbe zilikuwa tano ingawa wagombea walikuwa nane, wajumbe waliopita ni Amina Said alipata kura 32, Gudluck Masawe kura 31, Baraka Mwakisale kura 27, Boniface Yohana alipata kura 25 na Johnson Kashushura kura 24 huku Thabit Njaidi, Yahya Ally na Charles Mkunda kura hazikutosha.

Viongozi hao waliahidi kufanya kazi kwa kushirikiana bila kukiuka Katiba yao pamoja na ya Klabu ya Simba.

Post a Comment

 
Top