BOIPLUS SPORTS BLOG

KATIKA kuonyesha wameipania kuiangamiza Azam katika mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa kwenye dimba la Taifa disemba 12, Simba imeamua kujichimbia visiwani Zanzibar ambako imeweka kambi ya wiki mbili wakifanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki.


Katika mchezo wa jioni ya leo uliowakutanisha Wekundu hao na Kimbunga Fc inayoshiriki Ligi kuu visiwani humo, Simba imeisambaratisha timu hiyo kwa mabao 5-2 huku ikionyesha uwezo mkubwa.

Mabao ya Simba katika mchezo huo wa kujipima nguvu yalifungwa na Ibrahim Ajibu aliyefunga mawili, Mussa Mgosi, Hijja Ugando na Danny Lyanga.

 Simba itajitupa tena uwanjani siku ya jumapili kucheza mchezo wa pili wa kirafiki na timu ambayo bado haijatajwa ingawa Kombaini ya Unguja inapewa nafasi kubwa. 

Baada ya mchezo huo Simba imepanga kucheza mchezo mwingine mmoja kabla ya kurejea Dar kuivaa Azam

Post a Comment

 
Top