BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
UKURASA wa maisha ya Andrey Coutinho ndani ya Yanga ulishafungwa, unajua ambacho kilibakia?.
Ni ujio wa kiungo Issoufou Boubacar Garba 'Diego' anayekuja kuchukua nafasi yake.

Alfajiri ya leo kiungo huyo kutoka Niger anayesifikia kwa kulitumia ipasavyo guu lake la kushoto ametua nchini tayari kwa majaribio yatakayotoa taswira kama apewe mkataba au la.

Hizi hapa ni picha zake tatu akiwa anawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Post a Comment

 
Top