BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA mkuu wa Toto Africans, John Tegete amekiangalia kikosi cha Simba katika mechi yao ya juzi Jumamosi na kutamka kwamba Simba haina wachezaji wenye hadhi ya kuichezea timu hiyo kwani viwango vyao ni vya kawaida sana huku akisema uwezo wa wachezaji wa Simba kucheza ni dakika 15 pekee.


Tegete ametamka kauli hiyo baada ya Simba kukubali sare ya bao 1-1 na timu yake katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ingawa mashabiki wa Simba waliamini kwamba wangeshinda mechi hiyo.

"Simba haina wachezaji wenye viwango vya kuibeba timu hiyo bali ina wachezaji wenye majina tu, wengi uwezo wao ni mdogo na wanazidiwa hadi na vijana wangu, hawa si wachezaji wa kuichezea timu kubwa kama Simba, na hao wachezaji wao wa kigeni hawana kipya, hili ni tatizo ambalo litaisumbua sana Simba tena kwa kipindi kirefu.


"Wachezaji wa Simba wana uwezo wa kucheza dakika 15 tu za mwanzo baada ya hapo pumzi inakata, hilo ni tataizo ambalo wanatakiwa kufanyiwa kazi vinginevyo watakuwa wanafungwa kirahisi kila mechi," alisema Tegete.

Simba sasa inakabiliwa na mechi ngumu ya Kanda ya Ziwa dhidi ya Mwadui FC itakayochezwa Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga

Post a Comment

 
Top