BOIPLUS SPORTS BLOG

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limezitaka klabu zote nchini za  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kuheshimu utaratibu uliowekwa wa usajili na utekelezaji wake, kwani TFF haitapendelea klabu yoyote kukiuka katika suala hilo.


TFF inachukua fursa hii kuwakumbusha viongozi wote wa klabu kuhusu kalenda ya mwaka ya usajili ambayo ina vipindi viwili,

(i)  Dirisha Kubwa la Usajili  (Juni 15 – Agosti 20)

(ii)  Dirisha Dogo la Usajili (Novemba 15 – Disemba 15)

Baada ya usajili hufuatia kipindi cha pingamizi ambacho kuchukua wiki moja, kisha Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF kupitia pingamizi hizo na kupitisha usajili wa wachezaji wote waliosajiliwa.

Kipindi cha usajili wa dirisha dogo ulifunguliwa Novemba 15 na utafungwa kesho Jumanne, kipindi hiki hutumika kwa ajili ya uhamisho, kutangaza wachezaji wanaoachwa kwa mujibu wa kanuni, kutangaza wachezaji waliositishiwa mikataba na kipindi cha pingamizi ni Disemba 16 – 22 na kuthibitisha usajili Disemba 23, mwaka huu.

TFF inaziomba klabu kufuata utaratibu uliopo kikanuni katika shughuli za uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

Post a Comment

 
Top