BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
BASI la mabingwa wapya wa kombe la Chalenji, timu ya Taifa ya Uganda 'The Cranes', leo limehusika katika ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu watano.

Wachezaji wa Cranes ambao ndio kwanza wametoka kubeba ubingwa huo nchini Ethiopia, walikuwa wakisafiri kwa basi lao kutoka Soroti walikokwenda kumtembelea Rais Yoweri Museveni na kumuonyesha kombe hilo la Chalenji.Kwa mujibu wa Daily Monitor, polisi waliokuwepo eneo la tukio pamoja na mashuhuda wengine wamesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji wa hovyo wa madereva hao. 

Basi la Cranes liligongana na basi dogo la abiri aina ya Nissan maarufu kama Matatu ambapo licha ya watu watano waliokuwemo kwenye basi hilo dogo kupoteza maisha, watu wengine kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.

Cranes walichukua Ubingwa wa Chalenji baada ya kuwafunga Rwanda 'Amavubi'

Post a Comment

 
Top